PICHA:BALOZI SEIF AONGOZA KIKAO CHA KUANGALIA CHANGAMOTO ZA WAWEKEZAJI - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 20 July 2018

PICHA:BALOZI SEIF AONGOZA KIKAO CHA KUANGALIA CHANGAMOTO ZA WAWEKEZAJI


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wawekezaji wenye miradi ya Kiuchumi Zanzibar pamoja na Viongozi wa Serikali wa Mikoa, Wilaya na Taasisi zinazosimamia Sekta ya Utalii pamoja na Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar {ZIPAR}.

Kikao hicho kilikuwa na madhumuni ya kuangalia changamoto zinazowakumbwa Wawekezaji hao katika Mikoa na Wilaya walizowekeza Vitega Uchumi vyao.
Wakuu wa Mikoa na Wizaya za Kisiwa cha Unguja ni miongoni mwa walioshiriki Kikao cha Wawekezaji wenye miradi ya Kiuchumi Zanzibar  waliokutana Vuga Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
Baadhi ya Wawekezaji na watendaji wa Taasisi zinazosimamia Sekta ya Utalii pamoja na Uwekezaji Vitega Uchumi |{ZIPA}.
Wawekezaji tofauti waliowekeza Zanzibar  wakiwa makini kufuatilia mazungumzo ya Balozi Seif kujadili changamoto zinazowakumba katika kuendeleza Miradi yao Nchini.

Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment