PICHABALOZI SEIF ALLI IDDI ATEMBELEA JUMBA LA TRENI LILOPO DARAJANI Z'BAR. - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 20 July 2018

PICHABALOZI SEIF ALLI IDDI ATEMBELEA JUMBA LA TRENI LILOPO DARAJANI Z'BAR.

Muonekano wa Jumba la Treni darajani litavyokuwa likiwa katika hatua za mwisho za kukamilika matengenezo makubwa yanayofanywa chini ya Wahjandisi wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya CRJ kutoka China.
Baadhi ya Milango ya Maduka yaliyomo ndani ya Jumba la Treni Darajani  yanayosubiri kukamilika kuwekwa milango wakati wowote kuanzia sasa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akifanya ziara fupi ya kukagua maeneo mbali mbali yaliyomo ndani ya Jumba la Treni Darajani linalotarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Kaimu Meneja Mipango wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Ndugu Abdul -aziz Ibrahim Iddi akimueleza Balozi Seif hatua iliyofikia ya matengenezo makubwa ya Jumba la Treni Darajani.
Balozi Seif akielezea faraja yake kutokana na hatua kubwa iliyofikiwa ya matengenezo makubwa ya Jengo la Kibiashara Maarufu Jumba la Treni Darajani Mjini Zanzibar.
Balozi Seif akisisitiza umuhimu wa kuzingatia utunzaji wa mazingira katika eneo la Jumba la Treni Darajani ambalo ndilo sura halisi ya muonekano wa Mji wa Zanzibar.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
20/07/2018.

No comments:

Post a Comment