PERISIC, MANCHESTER, VIDA, MORATA: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO IJUMAA - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 27 July 2018

PERISIC, MANCHESTER, VIDA, MORATA: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO IJUMAA


Manchester United bado ina matumaini kusaini mkataba na winga wa Milan Ivan Perisic mwenye umri wa miaka 29 na itamuuza tu mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, mwenye umri wa miaka 22, ikiwa mchezaji huyo wa Croatian atapatikana. (Mirror)

Mlinzi wa Tottenham raia wa Ubelgiji Toby Alderweireld, mwenye umri wa miaka 29, amesalia kuwa ndiye anayepewa kipaumbele kusaini mkataba na Manchester United lakini the Londoners wanataka £55m au Anthony Martial ajumuishwe katika mazungumzo ya mkataba. (Independent)

Mmiliki wa Spurs Daniel Levy anaamini kuwa anaweza kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati wa Aston Villa Muingereza Jack Grealish, mwenye umri wa miaka 22, kwa £20m. (Mirror)

Liverpool hawana nia ya kusaini mkataba na mlinzi wa Besiktas Domagoj Vida, mwenye umri wa miaka 29,licha ya kuwa na uhusiano na timu ya taifa ya Croatia. (Liverpool Echo)

Chelsea imeiambia AC Milan ilipe hadi £62m ikiwa wanataka kusaini mkataba na mshambuliaji Muhispania Alvaro Morata mwenye umri wa miaka 25. (Sky Sports)

Maafisa wa Chelsea wamesafiri hadi Italia kusaini mkataba na mlinzi wa Juventus Daniele Rugani, mwenye umri wa miaka 23, lakini wanasitasita kutimiza kiwango cha thamani yake cha £40m (Times - subscription required)

Mmiliki wa Blues Roman Abramovich na mkurugenzi Marina Granovskaia watakutana mjini Nice kushauriana kuhusu malengo yao ya uhamisho wa wachezaji (Evening Standard)

Barcelona wako tayari kukubali pendekezo la Everton la kiwango cha £27m kumnunua mlinzi wa timu ya taifa ya Colombia Yerry Mina, mwenye umri wa miaka 23. (Goal)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment