Neymar afunguka mazito baada ya kuzidi kwa kejeli za kuwa anajiangusha Uwanjani - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 30 July 2018

Neymar afunguka mazito baada ya kuzidi kwa kejeli za kuwa anajiangusha Uwanjani

Mshambuliaji wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Brazil Neymar da Silva Santos Júnior (Neymar),amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya tuhuma zinazomkabili za kujidondosha dondosha Uwanjani hasa kwenye michuano ya kombe la Dunia. iliyofanyika Urusi 2018.
Neymar akiongea hayo kupitia tangazo lao na mdhamini wake na mtengenezaji wa bidhaa za huduma ya kibinafsi ya Gillette,na kukubaliana na yote yanayoendelea kuzungumzwa.
Neymar amekiri kuwa alipiga kelele wakati wa Kombe la Dunia lakini nyota huyo ameahidi kuwa mtu mpya baada ya kuanguka na kuonesha vitendo ambavyo havikuwaridhisha mashabiki katika michuano iliyofanyika huko Urusi.
Kulikuwa na matumaini makubwa kwa Neymar kuibeba timu yake ya Brazil katika michuano ya kombe la Dunia Urusi 2018 lakini mambo yalienda ndivyo sivyo katika robo-mwisho dhidi ya Ubelgiji.
“Unaweza kufikiria ninapindukia, na wakati mwingine mimi hujifanyisha. Lakini ukweli ni kwamba huwa nateseka sanaUwanjani.Ukiwa nje unaona kama najifanya lakini huwezi kuniamini”
“Ninapoondoka bila kuzungumza na waandishi wa habari, sio sababu ninapenda kushinda tu, ni kwa sababu bado sijajifunza na sipendi kuwakatisha mashabiki tamaa”
“Wakati naonekana nina kuwa hasira, sio sababu mimi ni mtoto bali ni kwa sababu sijajifunza jinsi ya kukabiliana na shida zangu pamoja na hasira zangu”
“Bado kuna Utoto ndani yangu.” Wakati mwingine najitahidi kupunguza kukimbizana na ulimwengu mara nyingine, huwa nafukuza kila mtu.Na vita yangu ni kumfanya huyu aendelee lakini ndani yangu, si ndani ya Uwanja”
“Nimetumia muda mwingi sana kukubaliana kejeli juu yangu,Pia nimetumia wakati mrefu mno wa kujiangalia kwenye kioo na kujiona nimekuwa mtu mpya,ndo mana niko hapa na moyo wangu ukiwa wazi na mweupe kabisa”
Kwa sasa Neymar anakipiga katika klabu ya PSG ya Ufaransa akisajiliwa msimu ulioita kutoka FC Barcelona kwa uhamisho uliovunja rekodi ya Dunia ya Euro 222 mil.

By Ally Juma.

No comments:

Post a Comment