- Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 24 July 2018


Na George Mganga

Baada ya hoja mbalimbali kutolewa na wadau wa soka nchini juu ya ongezeko la wachezaji wa kigeni kutoka 7 mpaka 10, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia, amelitolea ufafanuzi leo.

Rais Karia amesema kuwa klabu ndizo zilipendekea kuwe na ongezeko hilo na mwisho wa siku aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Clement Sanga, alikubali ombi hilo kupitia kikao walichokaa Juni 30 2018.

Baada ya mapendekezo hayo kupitishwa kunako Bodi ya Ligi, baadaye Kamati ya Utendaji ya TFF ilikaa na kuyajadili kisha kufikia mwafaka wa omgezeko hilo kupitishwa.

Hatua ya Karia kutolea ufafanuzi huo ni kutokana na baadhi ya malalamiko kutoka kwa wadau wa soka nchini kuanza kuhoji imekuwaje TFF imefikia uamuzi huo kuliko kujali vipaji vya wazawa kuvilinda.

Mapema baada ya ongezeko hilo kuwekwa hadharani, wengi walikuwa walifunguka na kueleza inaweza kuwa chanzo cha kuvunja ndoto za wazawa wengi kutoka kisoka baada ya idadi ya wageni kuwa wengi.

No comments:

Post a Comment