MUSIC AUDIO: R. Kelly aachia wimbo wa dakika 19 kuanika maovu yake, wadau wataka akamatwe na polisi - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 24 July 2018

MUSIC AUDIO: R. Kelly aachia wimbo wa dakika 19 kuanika maovu yake, wadau wataka akamatwe na polisi

Msanii mkongwe wa muziki wa R’n’B duniani, Robert Kelly maarufu kama R. Kelly ametumia dakika 19 kwenye wimbo wake mpya wa ‘I Admit’ kuweka wazi tuhuma za unyanyasaji wa kingono zilizokuwa zinamuandama kwa muda mrefu.

R. Kelly
Kwenye wimbo huo R. Kelly amekiri miaka ya nyuma kuwahi kutembea na rafiki wa karibu na GirlFriend pia kufanya mapenzi na mashabiki wake kila jiji aliloenda kutumbuiza kwa kipindi hicho.
Kwenye mashairi ya mwisho ya wimbo huo R. Kelly anasema kuwa kuna kipindi alikuwa anatembea na madada poa kwenye kumbi za starehe huku akimuacha mchumba wake nyumbani.
R. Kelly anasikika pia akisema anajutiakuishi maisha hayo ndio maana aka-Admit kuwa kuna mambo aliyoyafanya hayakuwa sawa ingawaje amefanya mambo mengine mazuri kama kuwasaidia wasanii wachanga ambao kwa sasa hivi wamefanikiwa kuliko yeye.
Pia ameomba msamaha kwa yote aliyowahi kuyafanya kwa mashabiki, Marafiki na ndugu zake kwani ni maisha ambayo kila akifikiria huwa anaumia sana.
R. Kelly miaka ya nyuma alishawahi kukumbwa na tetesi za unyanyasaji wa kingono kwa wasichana wenye umri mdogo Miaka 18 ambapo kwenye wimbo wa ‘I Admit’ amekiri kufanya maovu hayo.
SOMA NA HII – R. Kelly akana kunyanyasa wanawake
Baadhi ya wanamuziki na waandishi wa habari kupitia ukurasa wa Twitter wameshauri R. Kelly akamatwe na ashtakiwe kwani kuomba msamaha sio njia ya kumfanya awe salama ile hali amekiri kufanya kosa.

Hata hivyo kwenye wimbo huo amezungumzia pia kuhusu mkanda wake wa ngono uliowahi kuvuja miaka ya nyuma ambapo amesema Mwanasheria wake alijua kila kitu na ilikuwa ni kwa makusudi. Usikilize wimbo huo hapa chini

No comments:

Post a Comment