MCHEZAJI YANGA: SINA IMANI NA KIKOSI CHETU DHIDI YA GOR MAHIA - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 29 July 2018

MCHEZAJI YANGA: SINA IMANI NA KIKOSI CHETU DHIDI YA GOR MAHIA


Wakati Yanga ikishuka dimbani leo kucheza mchezo wa mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC, Mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Sekilojo Chambua amesema ana hana imani na wachezaji wa Yanga.

Chambua amefunguka na kusema kwa aina ya wachezaji Yanga ilionao kuna wasiwasi mkubwa wa kupata matokeo japo akieleza Kocha wake, Mwinyi Zahera, atakuwa amefanyia kazi mapungufu.

Mchezaji huyo aliyewahi kutamba miaka ya nyuma huku akitunza kumbukumbu zake nyingi katika mpira, amesema mapungufu ambayo Yanga walionesha katika mechi ya awali kule Nairobi yatakuwa yamerekebishwa na Zahera.

Kuelekea mechi hiyo, Chambua kwa upande mwingine anaimani kama Yanga wakipambana vilivyo wanaweza kupata matokeo kwa faida ya uwanja wa nyumbani.

Katika mechi ya awali iliyochezwa Nairobi wiki jana, Yanga ilikubali kichapo cha mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Mo Kasarani nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment