Matokeo ya vipimo vya afya ya Ronaldo yashtua wengi, yalingana na kijana wa miaka 20 - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 24 July 2018

Matokeo ya vipimo vya afya ya Ronaldo yashtua wengi, yalingana na kijana wa miaka 20

Klabu ya Juventus ya nchini Italia imetoa matokea ya vipimo vya afya vya mchezaji wao mpya, Cristiano Ronaldo ambaye wamemsajili kwaajili ya msimu mpya wa ligi na michuano mingine mbalimbali.
Juve ambayo imemsajili Ronaldo kwa dau la euro milioni 105  akitokea Real Madrid imeanika matokeo hayo ya vipimo vya nyota huyo ambavyo vimeonekana kuwa si vya kawaida kwa mtu mwenye umri mkubwa kama wake.
Kwa mujibu wa Matteo Bonetti matokeo ya utimamu wa mwili wa mshambuliaji huyo yaliyotoka yanalingana na kijana wa umri wa miaka 20.
Majibu yake yamesema kuwa ana 7 % ya kiwango cha mafuta mwilini tofauti na wachezaji wengine ambapo ni sawa na wastani wa 10 au 11% na 50% ya uwezo wa misuli yake jambo ambalo ni bora zaidi ukilinganisha na watu wenye umri kama wake.
Kama haitoshi nyota huyo mwenye umri wa miaka 33, ameweza kukimbia jumla ya kilomita 33.98 kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Urusi jambo ambalo linaendelea kuvunja rekodi kwa mtu mwenye umri kama wake.
Kwa mujibu wa gazeti la AS la nchini Hispania mnamo mwaka 2017, Ronaldo alikuwa na spidi ya kilomita 33.25 kwa saa huku akithibitisha utimamu wa mwili wake baada ya kuruka umbali wa mita 2.3 kwenda juu alipokuwa akisherehekea goli lake dhidi ya Juve michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Kabla ya kujiunga na vibibi hivyo vya Turin mapema mwezi huu, benchi la ufundi la Real Madrid limewahi kuripotiwa kuwa kwamujibu wa vipimo utimamu wa mwili wa Cristiano Ronaldo unalingana na kijana mwenye umri wa miaka 23 miaka mitatu iliyopita kabla hayajatoka majibu haya mapya kutoka klabu yake mpya ya Juve ambayo analingana na kijana mwenye miaka 20.
Mshindi huyo mara tano wa taji la Ballon d’Ors, Ronaldo amejiunga na Juve kwa kandarasi ya miaka minne akitokea Madrid.

No comments:

Post a Comment