Mapenzi yamemchanganya Chioma wa Davido Mpaka Kaacha Chuo? - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 27 July 2018

Mapenzi yamemchanganya Chioma wa Davido Mpaka Kaacha Chuo?

Tetesi zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusiana na mpenzi wa sasa wa superstar Davido ambaye ni Chioma kufikia maamuzi ya kuacha chuo na kuhamisha maisha yake katika mapenzi na staa huyo hii ni baada ya kuonekana kukosa vipindi darasani.

Inadaiwa kuwa baba yake Chioma ambaye ni mchungaji hajapendezwa na taarifa hizo za mtoto wake kukosa vipindi na kufikia maamuzi hayo ya kuacha chuo ikiwa Chioma ni mwanafunzi wa chuo cha Babcock kilichopo Nigeria na alikuwa akifanya course ya uchumi tokea 2012 na kusemekana kuwa alitakiwa kumaliza elimu hiyo mwaka 2016.Taarifa nyingine zinadai kuwa Chioma hajahudhuria masomo yake ndani ya mwezi mmoja katika chuo hicho na kuhusishwa  kuwa amekuwa na safari nyingi za nje na mpenzi wake Davido  huku marafiki zake wa karibu wakidai kuwa hawaoni dalili za Chioma luridi tena chuoni.Huku tuhuma zingine zikidai kuwa baba wa Chioma aliwahi kuzungumza naye na kumtaka mwanae amalize shule kwanza kabla hajajihusiha na ishu za ndoa na wengi wanaamini kuwa Chioma na Davido wanaishi kama wanandoa kwa sasa.

No comments:

Post a Comment