MANARA: KAMA UNATEGEMEA SIMBA KUFILISIKA, HILO HALIPO - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 25 July 2018

MANARA: KAMA UNATEGEMEA SIMBA KUFILISIKA, HILO HALIPO


Na George Mganga

Ofisa Habari wa Simba, Haji  Manara, amefunguka kueleza juu ya mwenendo wa klabu hiyo namna unavyoenda hivi sasa na matarajio ya baadaye.

Manara ameeleza Simba ya sasa inaenda vizuri kutokana na kuingia katika mabadiliko mapya na ya kisasa ya mfumo wa kiuendeshwaji na akisema watu wasitarajie kuiona ikirudi ilipotokea.

Manara ambaye huwa haishiwi maneno, amesema uwekezaji wa kiasi cha shilingi za kitanzania, bilioni 20 uliowekezwa na Mohammed Dewji ni mkubwa hivyo utaleta manufaa kwa Simba.

Ofisa huyo amesema Mo si mfadhili kama ilivyokuwa kwa wengine na badala yake ni Mwekezaji huku akieleza kama kuna watu wanatarajia Simba kufikrisika wasahau kabisa.

"Unajua kuna watu washachukulia kuwa uwekezaji ni sawa na ufadhili, Mo amewekeza bilioni 20 Simba hivyo wasitarajie kuona klabu inarudi ilipotoka hata kidogo" alisema.

No comments:

Post a Comment