Mama Kanumba amtaja Muigizaji aliyeziba pengo la mtoto wake kwenye tasnia ya filamu Tanzania - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 22 July 2018

Mama Kanumba amtaja Muigizaji aliyeziba pengo la mtoto wake kwenye tasnia ya filamu Tanzania

Mama mzazi wa aliyekuwa Muigizaji wa filamu maarufu zaidi Tanzania, Steven Kanumba amesema kuwa kwa sasa Watanzania wasiwe na hofu tena kwani anaamini kuna vipaji vikubwa kama alivyokuwa marehemu mtoto wake.

Mama Kanumba
Akizungumza na Wasafi TV kwenye usiku wa uzinduzi wa filamu ya SUMU Mlimani City jana Julai 21, 2018. Mama Kanumba amemtaja Muigizaji wa Kiume Gabo Zigamba kama ndiye msanii pekee mwenye uwezo sawa na Kanumba kwa sasa.
Akizungumzia uwezo wa Gabo Mama Kanumba amesema kuwa “Gabo anajitahidi kwa kweli, nilichogundua kwanza anajua kuuvaa uhusika kwenye filamu zake, akiwa kama mlinzi anakuwa mlinzi kweli, akiwa kichaa anakuwa kichaa kweli. Namwambia asikate tamaa kuna watu watamkatisha tamaa kila atapokaribia kuyafikia mafanikio zaidi.
Akifananisha uwezo wa Gabo na marehemu Kanumba, Mama Kanumba amesema “ni kweli Gabo ‘anashika kijiti cha Kanumba’ anajitahidi, anauthubutu, anajaribu, anajituma na anaweza”.
Marehemu Kanumba anatajwa kuwa ni moja ya Waigizaji bora wa muda wote kuwahi kutokea kwenye tasnia ya filamu nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment