Malcom akamilisha uhamisho wa kujiunga na Barcelona - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 28 July 2018

Malcom akamilisha uhamisho wa kujiunga na Barcelona


Winga wa Brazil Malcom amekamilisha uhamisho wa kitita cha £36.5m kwa kujiunga na Barcelona kutoka Bordeaux.

kwa mujibu wa BBC, Mkataba huo ulitangazwa mara ya kwanza siku ya Jumanne baada ya mabingwa hao wa Uhispania kuwashinda Roma katika kupata saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.

"Hii ni ndoto ya utotoni ambayo imetimia'', alisema Malcom, ambaye bado hajaichezea timu ya taifa ya Brazil .''Natamani kuanza kucheza''.

Roma inafikiria iwapo ina kesi ya kuwasilisha baada ya kuafikiana na Bordeaux siku ya Jumatatu, wakisubiri vipimo vya kimatibabu kufanywa.

''Najua ni changaomoto kuichezea Barcelona , lakini hii ni ndoto niliokuwa nayo tangu nikiwa mdogo'', alisema katika hafla ya vyombo vya habari ilioandaliwa na Barcelona inayoelekea Marekani.

Barcelona italazimika kulipa dau la awali la Yuro 41m huku kitita chengine cha Yuro milioni 1 tofauti kikitolewa.

No comments:

Post a Comment