MAJUTO KUOGA MAMILIONI - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 26 July 2018

MAJUTO KUOGA MAMILIONI

Tokeo la picha la MZEE MAJUTO
GOOD news! Msanii wa vichekesho Bongo, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ anatarajia kuanza kulipwa mamilioni ya fedha kutoka kwa watu walioingia naye mikataba isiyokuwa mizuri. Akizungumza na Amani Jumatatu iliyopita, nyumbani kwake, maeneo ya Bunju jijini Dar, Majuto alisema aliamua kusamehe ile mikataba midogomidogo ila kwenye ile mikataba mikubwa aliyodhulumiwa ambayo Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe aliahidi kumsaidia, ataendelea kusubiri kwani amepewa miezi miwili.
“Niliamua kusamehe ile mikataba yangu midogomidogo ila hiyo mingine aliyosema ataishughulikia muheshimiwa Mwakyembe bado naendelea kuisubiri ila kwa sasa siwezi nikaongea chochote kuhusu hilo, hivyo naomba mumuulize msemaji wa chama cha waigizaji,” alisema Majuto.Picha inayohusiana
Amani pia lilifanikiwa kuongea na msemaji wa Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni, Masoud Kaftany ambaye alisema hatua aliyofikia Mwakyembe ya ufuatiliaji wa mikataba ya wasanii akiwemo mzee Majuto inaendelea vizuri na hivi karibuni kila kitu kitakuwa sawa. “Hivi karibuni alizungumza kwamba tutegemee baada ya miezi miwili au mitatu suala la mzee Majuto, Steven Kanumba pamoja na Wastara Juma litakuwa limeshamalizika hiyo mikataba,” alisema Kaftany.

No comments:

Post a Comment