Mabadiliko ya JPM, awapa shavu wapinzani - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 28 July 2018

Mabadiliko ya JPM, awapa shavu wapinzani


Leo Julai 28 Rais John Magufuli amefanya uteuzi na mabadiliko ya viongozi wa Wizara, Mikoa na Wilaya mbalimbali nchini.

Akitangaza mabadiliko hayo Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini mwaka 2010-15 kwa tiketi ya Nccr-Mageuzi, David Kafulila kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe ambapo Novemba 24, 2017, Kafulila aliibukia kwenye mkutano wa kampeni wa CCM Kata ya Mbweni na kutangaza kujiunga na CCM alipoitwa jukwaani na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Hamphrey Polepole

Pia amemteua Moses Machali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu. Machali aliwahi kuwa mbunge wa Kasulu Mjini, (NCCR-Mageuzi) kabla ya kuhamia ACT-Wazalendo na baadaye CCM.

Kadhalika Rais Magufuli amemteua Patrobas Katambi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambapo awali alikuwa Mwenyekiti wa baraza la Vijana Chadema (BAVICHA).

Katambi alitangaza kujiondoa Chadema Novemba 21,2017 na kujiunga CCM, katika mkutano wa halmashauri kuu ya CCM ulioendeshwa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli jijini Dar es salaam.

Katambi alikuwa mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 akikabiliana na Stephen Masele (CCM) ambaye aliibuka mshindi huku Katambi akidai kuibiwa kura katika uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment