Liverpool wamtambulisha golikipa ghali zaidi duniani - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 20 July 2018

Liverpool wamtambulisha golikipa ghali zaidi dunianiDone Deal - Klabu ya soka ya Liverpool imekamilisha usajili wa golikipa Mbrazil Alisson Becker kutoka AS Roma kwa uhamisho wa paundi milioni 67.

Kiasi hicho cha fedha kinamfanya Alisson kuweka rekodi ya kuwa kipa aliyesajiliwa kwa fedha nyingi zaidi duniani.

Akiongea baada ya kutambulishwa kuwa mchezaji mpya wa Liverpool, kipa huyo amesema kutua kwake kwenye timu hiyo ya Uingereza ni ndoto ambayo imekuwa kweli katika maisha yake ya soka.

"Ninafuraha sana, ni ndoto ambayo imekuwa kweli kuvaa jezi ya kifahari kwa klabu hii kubwa ambayo hutumiwa kushinda daima. Kwa upande wa maisha yangu na kazi yangu, ni hatua kubwa kwangu kuwa sehemu ya klabu hii na familia hii. Unaweza kuwa na uhakika kwamba nitatoa mchango wangu wote," amesema Alisson.

No comments:

Post a Comment