Lionel Messi kutua Italia kumkabili Ronaldo ligi ya Serie A - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 24 July 2018

Lionel Messi kutua Italia kumkabili Ronaldo ligi ya Serie A

Vita ya wachezaji pendwa zaidi duniani katika soka, Cristiano Ronaldo na Lionel Messi haijafika mwisho baada ya wawili hao kuwa kwenye ligi tofauti.
Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi
Ronaldo aliyetoka Madrid na kusajiliwa na Juventus ya Italia baada ya utawala wake wa misimu tisa Laliga ameonekana kama ametengana na mpizani wake Messi aliyebaki nchini Hispania lakini kwa sasa mambo huwenda yakabadilika kwa wawili hao kukutana tena kwenye ligi moja ambayo ni Serie A ya nchini Italia.
Mshambuliaji wa Juventus, Cristiano Ronaldo
Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Italia klabu ya Inter Milan inahusishwa kutaka kumsajili mshambuliaji hatari wa Barcelona, Lionel Messi ili kuleta ushindani kwenye ligi ya Serie A dhidi ya Juventus ambao wamekamilisha dili la kuingia kandarasi na Cristiano Ronaldo.
Wadhamini wa kuu wa klabu ya Inter Milan ambao ni kampuni ya Pirelli kupitia Mkurugenzi mtendaji wake, Marco Tronchetti Provera katika mahojiano yake amesema kuwa mmiliki wa timu hiyo ambayo ni Suning ikiwa chini ya Zhang Jindong inatarajia kufanya usajili mkubwa mno kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Pirelli, Marco Tronchetti Provera
Tronchetti Provera katika mahojiano yake amekwenda mbali zaidi na kusema kuwa anaimani Suning inaweza kufanya usajili mkubwa sana na kuhoji kwa nini isiwezekane kuwa ni Messi.
Messi mwenye umri wa miaka 31, ameingia mkataba wa muda mrefu na klabu ya Barcelona unaomuweka hapo mpaka msimu wa mwaka 2021.

No comments:

Post a Comment