Leo ndio Leo, Inasemekana Mwezi Utapatwa Usiku Kwa Muda Mrefu Kuwahi Kutokea Duniani - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 27 July 2018

Leo ndio Leo, Inasemekana Mwezi Utapatwa Usiku Kwa Muda Mrefu Kuwahi Kutokea Duniani

Kama umefanikiwa kuiona Ijumaa ya leo Julai 27, 2018 basi mshukuru Mungu sana kwani umepata bahati ya kushuhudia tukio kubwa la kupatwa kwa mwezi usiku wa leo.


Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwenye Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) tukio hilo litatokea majira ya kuanzia saa 4:30 usiku hadi 6:14 .

Tukio la kupatwa kwa mwezi linatarajiwa kuonekana vizuri katika maeneo mengi ya bara la Afrika, Asia na Ulaya. Hapa nchini Tanzania tukio hilo linatarajiwa kuonekana katika maeneo mengi na linatarajiwa kudumu kwa takribani masaa mawili.

Kupatwa kwa Mwezi hutokea wakati Dunia, Mwezi na Jua vinapokuwa kwenye mstari mmoja. Hali hiyo inapotokea mwanga wa jua unaofika katika uso wa mwezi huzuiwa na duara la Dunia. Katika mpangilio huo nuru ya Mwezi huonekana kuwa na giza (Total Lunar Eclipse), hali inayotarajiwa kujitokeza katika maeneo ya bara la Afrika, Asia na Ulaya usiku wa leo tarehe 27 Julai 2018.

Kupatwa kwa Mwezi husababisha mabadiliko katika nuru ya mwezi na hivyo kufanya nuru ya mwezi kuwa hafifu(Partial Lunar Eclipse) au kuwa giza (Total Lunar Eclipse). Kwa kuwa kupatwa kwa mwezi kutatokea kipindi Mwezi ukiwa mbali zaidi na Dunia, inatarajiwa kuwa tukio hili litaonekana kwa muda mrefu zaidi ukilinganisha na matukio mengine katika karne ya 21.

No comments:

Post a Comment