Kundi la P Square litarudi endapo ndugu yangu atayaacha haya – Peter (P Square) - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 30 July 2018

Kundi la P Square litarudi endapo ndugu yangu atayaacha haya – Peter (P Square)

Peter Okoye alimaarufu Peter wa P Square amefunguka A-Z kuhusiana na chanzo cha kuvunjika kundi lao la P Square ambalo lilikuwa linaundwa na ndugu hao wawili ambao ni yeye Peter pamoja na pacha mwenzake Paul.
Peter ameongea hayo Jijini Nairobi chini Kenya katika ziara yake na kituo cha habari cha Citizen Tv na kusema mengi sana yaliyosababisha kundi hilo kuvunjika.Peter alisema:- “Paul Mara zote hakuheshimu familia yangu,na mimi nilijitolea kuwalinda”
Peter aliongeza:- Tumevunja kundi letu mara tatu na suala hilo liko bado,kama tutaamua kurudisha kundi hili itabidi kushughulikia suala hili,yote yanawezekana kuhusu kundi hili kurudi au kutokurudi.
Pia ameweka wazi juu ya kile kinachoendelea kwenye vichwa vya watu wengi kwamba nilijitoa kwa sababu sikuheshimiwa ni kweli maana kitendo hicho kilizidi na kilizidi hadi kwenye familia yangu.
“Kundi hili linaweza kurudi kama heshimu itakuwepo kwa asilimia 100,mimi naiheshimu sana familia ya kaka yangu lakini yeye hafanyi hivyo kwangu,yeye ataniongelea mimi kwenye mitandao ya kijamii lakini bado nitabaki kuwa ndugu yake,mimi nimejitahidi kumlinda mke wangu na watoto wangu ndo kitu ambacho nilikiahidi siku nafunga ndoa kuwa ntailinda na kuisimamia familia yangu”
Kundi la P Square liliundwa na ndugu wawili ambao ni Peter pamoja na pacha mwenzake Paul,ambalo linatokea nchini Nigeria.

By Ally Juma.

No comments:

Post a Comment