KIONGOZI YANGA ATAMBA KUWAMALIZA GOR MAHIA LEO, AWAKARIBISHA MASHABIKI KUMUONA STRAIKA HATARI MAKAMBO - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 29 July 2018

KIONGOZI YANGA ATAMBA KUWAMALIZA GOR MAHIA LEO, AWAKARIBISHA MASHABIKI KUMUONA STRAIKA HATARI MAKAMBO


Mwenyekiti wa Umoja wa Matawi Yanga nchini, Bakili Makele, ameibuka na kuja kitofauti zaidi kuhusiana na mchezo wa leo baina ya Yanga na Gor Mahia FC.

Mechi hiyo ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika itapigwa majira ya saa 1 jioni katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, leo.

Makele ametamba kwa kusema kwa kikosi cha Yanga kilivyo sasa kuna uhakika mkubwa wa kupindua matokeo dhidi ya wapinzani wao ambao walishinda mechi ya mkondo wa kwanza jijini Nairobi.

Makele ameeleza kuwa ongezeko la wachezaji kadhaa kuelekea mechi hiyo ikiwemo Deus Kaseke, Mateo Anthony pamoja na Kelvin Yondani aliyeongeza mkataba wa miaka miwili utaleta chachu ya ushindi.

Aidha, kwa upande mwingine Makele amewaomba wanachama na mashabiki wa Yanga waje kwa wingi Uwanjani ili wamuone straika hatari mpya, Heritier Makambo, ambaye amesajiliwa kutoka Congo.

Makele amesema Makambo ndiye mbadala wa Donald Ngoma hivi sasa ambaye aliondoka Yanga kwa kuvunja mkataba wake na kuelekea Azam FC ya jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment