Kiongozi mwingine mkubwa Yanga aachia ngazi - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 22 July 2018

Kiongozi mwingine mkubwa Yanga aachia ngazi


Hali ya klabu ya Yanga imeendelea kuwa si shwari ambapo taarifa zinaelezwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Khalfan Hamis ametangaza kujiuzulu wadhifa wake.

Taarifa inaeleza Hamis ameamua kuandika barua kwenda kwa Kaimu Mwenyekiti wa klabu, Clement Sanga akiomba kuachia ngazi kutokana na viongozi wa klabu hiyo kushindwa kufanya mambo kwa ueledi.

Barua hiyo imeeleza kuwa Yanga imekuwa na viongozi ambao wamekuwa hawaweki mambo sawa na badala yake kumekuwa na kificho bila kuweka kila kitu wazi kwa faida ya klabu.

Aidha imeelezwa kukosa ueledi kwa baadhi ya viongozi ni moja ya sababu tajwa ambazo zimeelezwa katika zilizoandikwa kwenye barua hiyo.

Sababu hizo ndizo zimepelekea kwa Hamis kuamua kuandika barua hiyo ya kuomba kujizulu ili kuwapa nafasi wengine.

Kuondoka kwa Hamis kumekuja baada ya siku kadhaa zilizopita kuelezwa kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Mkwasa naye ameachia wadhifa huo ndani ya Yanga.

No comments:

Post a Comment