Kevin Prince Boateng atangaza vita nchini Italia ‘Pengine mimi ndio Cristiano Ronaldo wa Sassuolo’ - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 25 July 2018

Kevin Prince Boateng atangaza vita nchini Italia ‘Pengine mimi ndio Cristiano Ronaldo wa Sassuolo’

Baada ya kukamilisha usajili wa miaka miwli ndani ya klabu ya Sassuolo ya Italia, Kevin Prince Boateng ametangaza vita na mshambuliaji hatari duniani, Cristiano Ronaldo.
Kufuatia ujio wa Ronaldo kwenye ligi ya Italia, kumemfanya mchezaji, Prince Boateng kupongeza zoezi hilo akiamini kuwa uwepo wa mshambuliaji huyo bora kabisa duniani atawezesha Serie A kuwa na ushindani mkubwa huku akiuliza je yeye ni Cristiano Ronaldo wa Sassuolo na kujijibu mwenyewe kuwa pengine ikawa hivyo.
Je mimi ni Cristiano Ronaldo wa Sassuolo, pengine ndio lakini nina magoli 500 tu. Nahitaji kumshinda lakini chakwanza lazima uishinde Juventus ambao wanawachezaji wengine waliyo bora.
Kwa upande wangu siwezi kumshinda Ronaldo peke yangu ninahitaji msaada wa wachezaji wenzangu. Usajili wake unaonyesha kwakiasi gani ligi hii ya Serie A ilivyo na umuhimu, yeye ni mchezaji bora duniani na amekuja hapa  ninaamini tutapata faida ya uwepo wake kwa vitu ambavyo havijapata kuonekana Italia.
Mchezaji huyo mwenye asili ya Ghana amesajiliwa Sassuolo kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Frankfurt nchini Ujerumani huku mpaka sasa akiwa ametupia mabao matano kwenye michezo yake miwili aliyocheza yakirafiki ya kujiandaa na msimu mpya waligi.

No comments:

Post a Comment