Kauli ya Coastal Union kuhusu kumsajili AliKiba - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 23 July 2018

Kauli ya Coastal Union kuhusu kumsajili AliKiba

Uongozi wa klabu ya Coastal Union ‘Wagosi wa kaya’ umefunguka na kuthibitisha kuwa katika mazungumzo na msanii wa Bongo Fleva, Alikiba ili waingie naye mkataba rasmi kwaajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara.

Hafidh Kido ambaye ni Afisa habari wa klabu hiyo amesema kuwa tetesi hizo kwa kiasi kidogo zina ukweli japo mambo bado hayajakaa sawa kiasi cha kuweza kutangazwa huku akikiri uwezo wa mchezaji huyo.

“Alikiba nadhani nyie wenyewe mnamuona uwezo wake sio wa kiwango cha juu ni kwasababu tu hana mazoezi  ya mara kwa mara na kucheza mechi, lakini Alikiba huwezi ukabeza kiwango chake hata siku moja“. Amesema Hafidh.

Kigezo kikubwa ambacho wanajadiliana na Alikiba ni jinsi gani mkataba wao utakavyokuwa kutokana na msaniii huyo kujihusisha kwa kiasi kikubwa katika kazi yake nyingine ya muziki.

Pia Hafidh amezungumzia kuhusu sababu ya wao kutotangaza usajili wowote mpaka sasa huku dirisha la usajili likielekea ukingoni wiki hii.

“ Usajili wetu bado, kocha anaendelea na uchambuzi wake na orodha ikishakamilika tutatangaza rasmi ili kuepuka migongano ya mikataba ya wachezaji na timu zingine, kwahiyo dirisha likikaribia kufungwa ndipo tutatangaza rasmi nani tunaye na nani hatunaye".

Coastal Union imepanda daraja msimu uliopita na sasa iko katika maandalizi rasmi Jijini Dar es Salaam ya msimu mpya wa ligi ambao unatarajia kutimua vumbi kuanzia Agosti 22 .

No comments:

Post a Comment