Jokate na Jarry Murro wala shavu la U-DC, Ally Hapi awa RC Iringa - Karafuu24 Blog

Breaking

Saturday, 28 July 2018

Jokate na Jarry Murro wala shavu la U-DC, Ally Hapi awa RC Iringa

Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa, wa wilaya na makatibu tawala nchini ambapo katika uteuzi wake, amemteua mwanamitindo Jokate Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe huku aliyekuwa msemaji wa Yanga, Jerry Murro kuwa mkuu wa wilaya ya Arumeru.
Katika uteuzi huyo pia, aliyekuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameteuliwa kuwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa na nafasi yake kuzibwa na Daniel Godfrey Chongolo.
Pia rais Magufuli akiwateua wanasiasa watatu waliowahi kuwa vyama vya upinzani katika nafasi hizo.
Amemteua David Kafulila kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe. Kafulila aliwahi kuwa mbunge wa NCCR-Mageuzi kabla ya kuhamia CCM.

No comments:

Post a Comment