Jeneza la ajabu lililogunduliwa Alexandria, Misri lafunguliwa - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 20 July 2018

Jeneza la ajabu lililogunduliwa Alexandria, Misri lafunguliwa

Wiki tatu zilizopita, wanaakiolojia nchini Misri waligundua jeneza kubwa lililoundwa kwa mawe magumu ya matale (granite) ya rangi nyeusi katika mji wa Alexandria.

Jeneza hilo lilikuwa limekaa kwa zaidi ya miaka 2,000 bila kufunguliwa.

Uvumi ulianza kueneza upesi, kwamba huenda jeneza hilo lilikuwa na mabaki ya kiongozi maarufu wa Wagiriki, Alexander the Great, au pengine kitu cha laanakubwa.

Kwa mujibu wa wataalamu waliolofungua, jeneza hilo halikuwa na hata kimoja kati ya vitu hivyo viwili.

Badala yake, waligundua mifupa ya watu watatu na maji machafu sana ya rangi ya hudhurungi ambayo yalitoa uvundo usioweza kuvumiliwa, mkali ajabu.

Waziri wa Vitu vya Kale wa Misri alikuwa ameteua kamati ya wanaakiolojia wa kufungua jeneza hilo ambalo liligunduliwa katika eneo kulikokuwa kunafanyika ujenzi.


Kwa mujibu wa kituo cha habari cha El-Watan cha Misri, awali walijaribu kuinua kifuniko cha jeneza hilo hadi sentimeta tano hivi juu (inchi 2), lakini uvundo wa ajabu uliwazuia kuendelea na kulazimika kuondoka eneo hilo.

Baadaye walilifungua, wakiwa wamejiandaa kwa vifaaa, wakisaidiwa na wahandisi kutoka kwa jeshi la Misri.

"Tuliipata mifupa ya watu watatu, na inaonekana ni kama walikuwa wa familia moja... Kwa bahati mbaya, miili hiyo haikuhifadhiwa katika hali nzuri na ni mifupa pekee iliyosalia," amesema Mostafa Waziri, secretary-general of the Supreme Council of Antiquities.

Jeneza hilo lilipatikana na mifupa ya watu watatu, wanaoaminika kuwa maafisa wa jeshi wa kale
Akizungumzia wasiwasi uliokuwa umeenea kwenye vyombo vya habari kwamba kufunguliwa kwa jeneza hilo pengine kungesababisha laana kutoka kwa Mafirauni, Bw Waziri alisema: "Tumelifungua na, namshukuru Mungu, kwamba hakujawa na giza duniani.

"Nilikuwa wa kwanza kutazama ndani ya jeneza hilo ... na niko hapa, nimesimama mbele yenu... na niko salama."

Licha ya hayo, eneo lilikopatikana jeneza hilo watu wamehamishwa huku kukiwa na wasiwasi kwamba linaweza kutoa hewa yenye sumu, gazeti la serikali ya Misri la Al-Ahram limeripoti.

Majeneza na makaburi ya kale ni hatari?
Wanasayansi wamefanikiwa kuthibitishakwamba hakuna "Laana ya Miili ya Kale", lakini je kuna hatari nyingine katika makaburi na majeneza ya kale?

Lodi Carnarvon, aliyefadhili ufukuaji wa makaburi ya Firauni Tutankhamun alifariki baada ya kuumwa na mbu muda mfupi baada yake kufungua kaburi hilo 1923.

Tangu wakati huo, kumekuwepo na uvumi kwamba kuvu au bakteria zilinusurika ndani ya kaburi hilo na kwamba zilimwambukiza nakusabaisha kifo chake.


Lakini F DeWolfe Miller, profesa wa utaalamu wa viini vinavyosabbaisha magonjwa Chuo Kikuu cha Hawaii ameambia National Geographic kwamba hakuna hatari yoyote.

"Hatujafahamu kuhusu kisa hata kimoja cha mwanaakiolojia au mtalii aliyewahi kuathirika [kutokana na bakteria au kuvu kutoka makaburisni]," aliambia jarida hilo.

Wataalamu wanasema watu hao watatu ambao mabaki yao yalipatikana Alexandria huenda alikuwa wanajeshi enzi za Mafirauni.

Fuvu la kichwa la mmoja wao lina nyufa zinazoashiria jeraha la mshale.

Sanamu ndogo ya alabasta ambalo ni jiwe jeupe laini lililofanana na marumaru ambayo imeharibika kiasi cha kutojulikana ilikuwa sanamu ya nini, pia ilipatikana pamoja na jeneza hilo.

Wataalamu walivalia barakoa wakilifungua jeneza hilo, ambalo lilitoa uvundo wa ajabu
Jeneza hilo lina urefu wa karibu mita mbili (futi 6.5) kwenda juu na urefu wa mita tatu, na ndilo kubwa zaidi la aina yake kuwahi kugunduliwa.

Lina uzani wa tani 27 na linaaminika kuwa la enzi za Wagiriki wafahamikao kama Ptolemy ambao ulianza mwaka 323 baada ya kifo cha Alexander the Great.

Wanaakiolojia sasa watachunguza jeneza hilo kwa kina kubaini waliozikwa humo ndani walikuwa wanaishi wakati gani na waliishi vipi.

No comments:

Post a Comment