Hii ndio show kali zaidi ya Diamond Platnumz kuwahi kutokea, awaimbisha kiswahili Wafaransa kisiwani Mayotte (picha+video) - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 29 July 2018

Hii ndio show kali zaidi ya Diamond Platnumz kuwahi kutokea, awaimbisha kiswahili Wafaransa kisiwani Mayotte (picha+video)


Diamond Platnumz
Kwa sasa ukitaja majina ya wasanii 10 bora wanaofanya vizuri barani Afrika huwezi kuacha kumtaja Diamond Platnumz hii ni kutokana na kuongezeka kwa wigo mpana wa mashabiki wake.

Hili la kuongezeka kwa idadai ya mashabiki linajidhihirisha hata pale Diamond anapokuwa nje ya Tanzania hususani katika mataifa ambayo hayaongei Kiswahili.
Jana Julai 28, 2018 Diamond Platnumz alikuwa katika visiwa vya Mayotte nchini Ufaransa ambapo aliweza kutumbuiza nyimbo zake zote tena zile ambazo hajafanya kolabo na jambo la kufurahisha licha ya asilimia 99% ya wananchi wa Mayotte kuzungumza Kifaransa lakini waliweza kuimba naye nyimbo zote kwa kiswahili.No comments:

Post a Comment