HIGUAIN, MARTIAL, WILLIAN, ALCANTARA: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 25 July 2018

HIGUAIN, MARTIAL, WILLIAN, ALCANTARA: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO JUMATANO


Real Madrid inajiandaa kutoa dau la £60m kumnunua mlinda lango wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris, 31. (Sun)

Bilionea wa Urusi Alisher Usmanov anataka kuuza asilimia 30 ya hisa zake katika klabu ya Arsenal baada ya kukiri kwamba mmiliki mkuu wa klabu hiyo Stan Kroenke hatomwachia udhibiti wa klabu hiyo. (Financial Times)

Manchester United na Chelsea zimewasilisha ombi la kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uhispania Thiago Alcantara, 27, ambaye anapatikana kwa dau la £62m. (ESPN)

United pia inajiandaa kuwasaini mchezaji mbadala wa winga wa Chelsea na Brazil Willian,kupitia winga wa croatia na Eintracht FrankfurtAnte Rebic, 24. (Independent)

Tottenham na Chelsea huenda zikamnyatia winga wa Ufaransa Anthony Martial, 22, ambaye anataka kuondoka katika klabu ya Manchester United lakini kusalia katika ligi ya Premia. (Sun)

Chelsea huenda ikamkosa mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 30, huku wapinzani wao wa Serie A AC Milan wakiwa na hamu ya kumsajili raia huyo wa Argentina kwa dau la £57m. (Evening Standard)

Chelsea inakaribia kumsaini mlinda lango wa siku nyingi wa Uingereza Robert Green, 38, kama nguvu mpya kwa uhamnisho wa bure. (Sun)

Fulham imekubali makubaliano ya kumsaini mchezaji wa Ujerumani na winga wa zamani wa Chelsea Andre Schurrle, 27, kutoka Borussia Dortmund. (West London Sport)

Liverpool itamzuia mshambuliaji Daniel Sturridge, 28, msimu huu na iko tayari kumpoteza mchezaji huyo wa Uingereza msimu ujao kwa uhamisho wa bure (Liverpool Echo)

No comments:

Post a Comment