Harmorapa yamemkuta haya baada ya kuvuja video zake za faragha mtandaoni - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 24 July 2018

Harmorapa yamemkuta haya baada ya kuvuja video zake za faragha mtandaoni

Msanii wa muziki Harmorapa amewaomba radhi watanzania baada ya kusambaa mtandaoni video zinazomuonyesha akiwa na anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake kitandani.
Harmo ameiambia Bongo5 kwamba ameanza kupokea simu nyingi hukusiana na video hizo huku akidai kwamba pia kuna taarifa amezipata kwamba TCRA wanaweza kumchukulia hatua kali za kisheria kwa kufanya kosa ilo.
Rapa huyo amedai video hizo ziliandaliwa kwaajili ya movie lakini anashangaa mwanadada aliyefanya naye ameamua kuzisambaza mtandaoni bila kushauri naye chochote.
“Ustaarabu haununuliwi wala hauazimwi sidhani kama kuna shule au chuo cha ustaarabu na kuwa kimya sana sio chanzo cha kunichafua au kutembelea nyota yangu. Naheshimu sana Idara za Mawasiliano Nchini (TCRA),  Napenda hata siku moja nije nishikane mkono na Waziri Mwakyembe au Muheshimiwa Raisi wetu Magufuli kwa kuwa msanii bora mwenye nidhamu TANZANIA ,” aliandika rapa huyo Instagram.
Aliongeza, “Picha na video zinazo sambaa eti mimi kuwa na Dada mmoja ambae sina uhakika kama namjua sana ila tulikutana katika kazi ya sanaa nilioshirikishwa na Watu ninao waheshimu tena sio wa nchi hii…. Huko MWANZA . kuchukua video ambazo sio Rasmi ukazipost kwa manufaa yako huo ni ..USHAMBA.. . Nasema mimi sio TYPE yako na sina mpango wa Kufunga Harusi na wewe…. Ungekua mjanja unge heshimu kazi kwanza tuliokubaliana na kuifanya. Mwisho napenda kuomba Radhi kwa Mashabiki wangu kwa Video zilizosambaa mimi nikiwa Chumbani nasisitiza ile ni Muve tena kubwa sana haikuwahi kutokea hapa Bongo …itapofika wenyewe kuitoa mtaamini nisemacho.,”
Rapa huyo ameiambia Bongo5 kwamba sasa anafanya jitihada za kuwatafuta wanasheria kwaajili ya kuliangia suala hilo ili apate haki yake.

No comments:

Post a Comment