HARMONIZE ASEPA NA KIJIJI KENYA - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 24 July 2018

HARMONIZE ASEPA NA KIJIJI KENYAKwa sasa Harmonize ameonekana kuiva tena ni moto wa kuotea mbali - Anauwezo wa kukusanya kijijikwenye show yoyote akiwa mwenyewe.

Msanii huyo wa WCB amewasha moto wa kufa mtu mjini Nairobi, Kenya kwenye show yake ya Koroga Festival ambayo imefanyika Jumamosi iliyopita na kukusanya nyomi la watu.

Kupitia video ya show hiyo ambayo Harmo ameiweka kwenye mtandao wa Instagram, alionekana kupokelewa kwa shangwe kubwa kutokaq kwa mashabiki huku wengine wakitokwa na machozi ya furaha."East African Young Star 🇰🇪💖 God bless everyone who made this ....!!! 🙏 #KONDEBOY 🌍," ameandika muimbaji huyo kwenye video hiyo.

Naye Diamond Platnumz alishindwa kuvumilia hisia zake kupitia video hiyo ambayo pia ameiweka kwenye mtandao huo ameandika, "@harmonize_tz in NAIROBI!! Damn! Always Making @wcb_wasafi PROUD!!...Mwenyez Mungu Tunakushuru kwa kuendelea Kubariki kidogo chetu...Tunashkuru kwa Upendo wa watu kwetu, Tunaomba Uwazidishie kila jema Waliombalo Mashabiki zetu Wanaotusapoti Usiku na Mchana!!... "

No comments:

Post a Comment