Harmonize ampost Harmorapa na Harmo Junior “God bless my twins brothers” - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 24 July 2018

Harmonize ampost Harmorapa na Harmo Junior “God bless my twins brothers”

Kwa mara ya kwanza muimbaji kutoka WCB, Harmonize ameamua kumpost Harmorapa pamoja na Harmo Junior wasanii ambao wanatumia sehemu ya jina la muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Kwangwaru.
Wawili hao kila mmoja tayari ameweza kujitapia mafanikio kimuziki kupitia majina hayo.
Jumanne hii Harmonize ameamua kuweka wazi namna anavyowachukulia vijana hao huku akidai kwamba kitendo hicho kinaonyesha ni jinsi mafanikio yake yalivyoweza kuwasaidai vijana wengine ambao walikuwa hawana mbele wala nyuma.

Ujumbe wa Harmonize, “Mwiko kukata Tamaa ama kukatishwa na mtu yeyote yule katika safari yako ya mafanikio hii safari ni ndefu sana….!!! Utakutana na changamoto nyingi mno….!!! yakiwemo matusi, dharau, uonevu, chuki, namengine kibao ila pale utakapokubali kukata tamaa ama kukatishwa utakuwa umewavunja moyo watu wengi sana….!!!! (1) familia yako (2) ndugu jamaa na marafiki( 3) hata wale wachache waliokuwa wanakutia Moyo na motisha uongeze jitihada nawengine wengi mno….!!! Itakuwa umewavunja moyo …!! lakini pia M/mungu ni waajabu na hajawahi kukosea katika hii Dunia kila alifanyalo lina maana. Kubwa sana..!!! Wenda kawaumbe Binadam wengine kwa mfano wako nikiwa namaana mnafanana ambalo ni jambo la heri na baraka 🙏 so ukikata tamaa nao pia utakuwa umewaangusha jitihadazako, maarifa, kuzishinda changamoto ndio njia peke inaweza kuleta faraja kwa wengi wanao kuzunguka zingatia hili 👉 #MaishaNiKombolela….!!! God bless my twins brothers 🙏🙏
Mashabiki wengi wamempongeza muimbaji huyo kwa kitendo hicho huku wengi wakimshauri asisite kuwasaidia zaidi kama atapata nafasi.

No comments:

Post a Comment