Haji Manara Afunguka Kuhusu Maamuzi ya Sanga Kuondoka Yanga - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 24 July 2018

Haji Manara Afunguka Kuhusu Maamuzi ya Sanga Kuondoka Yanga

Baada ya Clement Sanga kujivua nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga jana, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amefunguka na kueleza namna alivyoguswa juu ya maamuzi hayo.

Manara amefunguka na kutoa pole kwa Sanga kutokana na vitisho alivyopewa na baadhi ya watu waliosema wataenda kumvamia nyumbani kwake kwa madai ya kuwa Yanga haitendei haki.

Ofisa huyo wa Simba ameeleza kuwa siku zote hakuna Yanga imara bila Simba na Simba imara bila Yanga kutokana na upinzani wa aina yake kwa timu hizo pindi zinapokutana Uwanjani.

Manara amesema pale Simba inapoifunga Yanga ikiwa na kikosi kipana Uwanjani na ipo vizuri hupata nguvu za kujitamba vizuri tofauti na hali waliyonayo sasa hata kama wakiifunga hawatakuwa na ubavu wa kujionesha kuwa ni bora zaidi.

"Unajua ukiifunga Yanga ikiwa katika ubora wake unapata nguvu za kutamba zaidi mtaani na kujiona wewe ndiyo kila kitu, lakini sasa kwa mwenedno walionao hata kama tukiwafunga, tutakuwa tumeifunga Yanga ambayo si bora na mbwembwe za kutamba hazitokuwepo" alisema.

No comments:

Post a Comment