DILUNGA AELEZA ATAKACHOKIFANYA ENDAPO ATAFANIKIWA KUTUA SIMBA - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 25 July 2018

DILUNGA AELEZA ATAKACHOKIFANYA ENDAPO ATAFANIKIWA KUTUA SIMBA


Kiungo wa Mtibwa Sugar, Hassan Dilunga, amesema hana wasiwasi endapo atafanikiwa kusajiliwa na mabosi wa Simba baada ya tetesi za muda mrefu.

Kwa muibu wa Radio One, Dilunga ambaye inaonekana bado hajafikia pazuri kimazungumzo na Simba, ameeleza anaamini atapata nafasi endapo atasajiliwa na klabu hiyo inayoteka vyombo vingi vya habari nchini kutokana na kuingia katika mfumo mpya wa mabadiliko.

Kiungo huyo ambaye ni moja ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha Mtibwa Sugar, anaamini ataweza kupata nafasi licha ya uwepo wa viungo wengi ambao wako kwenye fomu kwa wekundu hao wa Msimbazi.

Tetesi za Dilunga kuhusishwa na Simba zimeanza muda mrefu na inaonekana kuna mazungumzo yanaendelea baina ya pande mbili kati yake na Simba japo mambo hajayaiva.

No comments:

Post a Comment