Diamond Akapimwe Akili na Kufanyiwa Maombi, Ametuabisha vya Kutosha -Dudubaya - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 27 July 2018

Diamond Akapimwe Akili na Kufanyiwa Maombi, Ametuabisha vya Kutosha -Dudubaya

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva DuduBaya amemwagia povu zito msanii mwenzake Diamond Platnumz baada ya kuvaa kikuku na kumtaka akapimwe akili.

Wiki chache zilizopita Diamond alizua gumzo Kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuposti picha yake aliyomuonyesha akiwa amevaa cheni ya mguuni (kikuku) ambayo inavaliwa mara nyingi na wanawake tu.Dudubaya amefunguka n kumtolea povu zito Diamond ambapo Kwenye Interview yake na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, amedai kitendo alichofanya Diamond ni cha kutia aibu kwa wanabongo fleva wote:

Kwa mdogo wangu Diamond kuvaa kikuku siwezi kujua anatangaza biashara gani hasa labda na yeye anatangaza biashara sawa sawa na wanawake wanaojiuza wanavyojitangaza kwa kuvaa kikuku kwaiyo kwa mimi ni aibu na  kaitia aibu Bongo fleva na hata familia yake na hata mademu zake anaolala nao hawana akili kwa nini wasimshauri asivae kikuku”.

Lakini pia Dudubaya aliendelea kumwaga povu na kumtaka Msanii huyo akapimwe akili:

Mimi naona akapimwe akili yake na pia akae chini na viongozi wa dini ili waweze kumpa ushauri”.

No comments:

Post a Comment