Coastal Union yathibitisha kumnasa Ali Kiba - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 26 July 2018

Coastal Union yathibitisha kumnasa Ali Kiba


Yakiwa yamebakia masaa machache kabla ya kufungwa dirisha la usajili kwa vilabu vya Ligi kuu, ligi daraja la kwanza pamoja na ligi daraja la Pili vilabu vingi vimeonekana kukamilisha usajili wake mapema huku vilabu vingine vikiwa bado havijakamilisha zoezi.

Kwaupande wa Timu ya Coastal Union ya jijini Tanga ambayo imepanda kushiriki ligi kuu msimu ujao, wao wanaendelea na usajili lakini wameahidi kutaja kikosi kilichosajiliwa na walioachwa mara baada ya kukamilika kwa usajili huku wakiweka wazi kuwa ni kweli wamemsajili msanii wa muziki nchini, Ali Kiba.

Ni masaa machache yakiwa yamebakia ambapo Mfumo mpya wa usajili wa TFF FIFA CONNECT unaendelea kufanya kazi ambapo timu mbalimbali zinapaswa kuhakikisha wanatimiza ndani ya mda uliopangwa.

Klabu ya Yanga ambayo ilionekana kusuasua katika suala la usajili, kwa sasa wanaonekana wanaelekea katika hatua ya mwisho kukamilisha, ambapo katika mazoezi ya hii leo wameonekana wachezaji mbalimbali akiwemo mlinda mlango Levy Matami kutoka TP Mazembe ya DR Congo. Mlinda mlango huyu anatajwa kuja kuchukua nafasi ya Rpstad Youth anayetajwa kupelekwa kwa Mkopo African lyon.

Pia ndani ya timu ya Yanga, unatajwa usajili wa mchezaji Herith Makambo kutoka nchini Ghana, huku wengine wakiwa katika majaribio akiwemo mlinda mlango kutoka TP Mazembe, Mtanzania Hamis Mroki pamoja na wachezaji wengine wawili mmoja akiwa raia wa Congo na mwingine kutoka Afrika Kusini.

Kwaupande wa Tanzania Prisons yenye makazi yake jijini Mbeya, wao wameweka wazi kuwa walishawatoa wachezaji watatu akiwemo Mohamed Rashid ambaye yupo Simba, Eliuta Mpepo pamoja na Kazungu Mashauri ambao wameenda kuitumikia Singida United .

Kwaupande wa Azam FC wao walishatangaza kuwatoa kwa mkopo wachezaji takribani nane kwenda Vilabu vya Ligi kuu pamoja na Ligi Daraja la kwanza.

Hizo ni baadhi ya timu lakini tutaendelea kukujuza mara baada ya dirisha kufungwa rasmi ambapo TFF walishatoa taarifa kwa vilabu kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza na kwa taarifa za mwisho ilionyesha ni timu mbili pekee za KMC na African lyon ndizo hazijakamilisha usajili wake

No comments:

Post a Comment