Chelsea kumjengea chumba cha kuvutia sigara Sarri - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 24 July 2018

Chelsea kumjengea chumba cha kuvutia sigara Sarri


Uongozi wa klabu ya Chelsea utalazimika kumtengea kocha wake mpya, Maurizio Sarri chumba maalumu cha kuvutia sigara ili kumwezesha kuifanya kazi yake vizuri klabuni hapo kutokana na kocha huyo kuwa mvutaji mkubwa na hawezi kufanya kazi bila vizuri bila kutumia sigara.

Sarri amekuwa maarufu kwa uvutaji sigara akiwa na klabu yake ya zamani ya  Napoli hadi katika eneo la uwanja, lakini nchini Uingereza uvutaji wa sigara sehemu za kazi ulipigwa marufuku mwaka 2006, sheria ambayo baadae ilihusisha hadi katika viwanja vya soka.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 59 anavuta sigara takribani 80 kwa siku huku akivuta sigara nne au tano kwa saa kulingana nataarifa za watu wake wa karibu,  hivyo Chelsea itawalazimu kumtengea eneo maalumu au chumba cha kuvutia sigara katika uwanja wake wa nyumbani kuepusha kuvuta katika hadhara ya watu.

Chelsea itacheza mchezo wake wa kwanza wa nyumbani Agosti 18 watakapowakaribisha Arsenal katika dimba la Stamford Bridge.

Mfahamu kwa ufupi Sarri

Maurizio Sarri ni kocha wa kiitaliano aliyezaliwa Januari, 1959 ambaye hakuwahi kucheza soka la kiushindani katika maisha yake, katika enzi za uchezaji wake alicheza katika nafasi ya ulinzi .

Alianza kazi ya kufundisha soka wakati akiwa mfanyakazi wa benki nchini Italia kabla ya kujiunga kwenye Serie B katika klabu ya Pescara mwaka 2005. Mwaka 2014 aliipandisha klabu ya Empoli katika Serie A, na kuiwezesha kumaliza katika nafasi ya juu kwenye msimu huo ndipo alipoajiriwa na Napoli.

Akiwa Napoli alifanikiwa kushinda tuzo kadhaa binafsi na mafanikio makubwa kwa klabu hiyo chini yake ni kumaliza katika nafasi ya pili msimu 2017/18 nyuma ya mabingwa Juventus, baada ya msimu kumalizika ndipo Chelsea ikamsajili kwa mkataba wa miaka mitatu.

No comments:

Post a Comment