CHELSEA, BARCELONA, MADRID, MANCHESTER, CAVANI, THIBAUT: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 26 July 2018

CHELSEA, BARCELONA, MADRID, MANCHESTER, CAVANI, THIBAUT: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO


Real Madrid huenda ikawasilisha dau la £89m ili kumnunua mshambuliaji wa PSG na Uruguay Edinson Cavani, 31, ili kuchukua mahala pake Cristiano Ronaldo, ambaye alijiunga na Juventus. (AS - in Spanish)

Manchester United wameambia Leicester City wanataka kumsaini beki wa Uingereza Harry Maguire ,25, mwenye thamani ya £65m. (Mirror)

United wamewasilisha ombi la kutaka kumsaini winga wa Eintracht Frankfurt mwenye umri wa miaka 24 Ante Rebic. (Mail)

Liverpool wamekubali mkataba wa miaka miwili na beki wa Croatia Domagoj Vida, 29, lakini atalazimika kununuliwa kwa bei ya Besikitas ya £22m . (A Spor - in Turkish)

Real Madrid imeingia katika makubaliano na kipa wa Chelsea na Ubelgiji Thibaut Courtois,26. (Mail)

Chelsea na Roma wanashindana katika kumsajili winga wa Jamaica Leon Bailey, 20, kutoka klabu ya Bayer Leverkusen. (Evening Standard)

Chelsea inachunguza kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, kwa lengo la kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 . (Independent)

Mkurugenzi wa Everton Marcel Brands ameelekea Barcelona ili kuendelea na mazungumzo ya kumnunua beki wa Colombia Yerry Mina, 23, na beki wa Ufaransa Lucas Digne, 25. (Mail)

Klabu mpya ilioteuliwa kucheza ligi ya Premia Wolves pia wamewasilisha ombi la kutaka kumsaini Mina kutoka Barcelona. (Sky Sports)

Wolves imewasilisha ombi la dau la £18m ili kumsaijili winga wa Uhispania Adama Traore, 22, kutoka timu ya ligi ya mabingwa Middlesbrough. (Sun)

Crystal Palace inafanya mazungumzo ya kumsaini kiungo wa kati wa West Ham na Senegal Cheikhou Kouyate, 28, kwa dau la £10m. (Sky Sports)

Serena Williams alalama kuhusu kufanyiwa vipimo vya 'kibaguzi'
Newcastle inakaribia kumsaini mshambuliaji wa klabu ya Mainz na Japan mwenye umri wa miaka 26 Yoshinori Muto. (Kicker - in German)

Kutoka BBC

No comments:

Post a Comment