BREAKING: Mauaji ya Bilionea Msuya Watu watano wahukumiwa kunyongwa hadi kufa - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 23 July 2018

BREAKING: Mauaji ya Bilionea Msuya Watu watano wahukumiwa kunyongwa hadi kufa


Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda Moshi imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa washtakiwa watano waliotekeleza mauji ya kukusudia ya mfanyabiashara wa Arusha, Mirerani, bilionea Erasto Msuya.

Washtakiwa hao waliohukumiwa adhabu hiyo ni Sharifu Mohamed, Karim Kuhundwa, Sadick Mohamed, Ally Majeshi na Mussa Mangu.

Hukumu hiyo imetolewa leo Julai 23, 2018 na Jaji Salma Maghimbi huku akimuachia huru mtuhumiwa mmoja wa kesi hiyo aliyejulikana kwa jina la Shwaibu Jumanne baada ya kukosekana ushahidi dhidi yake.

Bilionea Msuya alikuwa akimiliki vitega uchumi kadhaa ndani na nje ya Arusha, aliuawa Agosti 7, mwaka 2013 kwa kutumia bunduki ya kivita ya Sub Machine Gun 'SMG' katika eneo la Mijohoroni Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro kwa kupigwa risasi sehemu mbalimbali za mwili wake.

Ilipofika Agosti 11, 2013 Jeshi la Polisi lilitangaza kuwakamatwa washukiwa muhimu wakihusishwa katika mtandao wa wahalifu waliofanya mauaji hayo na kupelekwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 21, 2013.

No comments:

Post a Comment