Askari Waliokamatwa Wakihusishwa na Kifo cha Akwilina Waachiwa Huru - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 24 July 2018

Askari Waliokamatwa Wakihusishwa na Kifo cha Akwilina Waachiwa HuruKamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa: amesema kuwa Askari waliokamatwa wakihusishwa na kifo cha mwanafunzi Akwilina Akwilini wameachiwa huru

Akwilina aliyekuwa Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji NIT aliuawa kwa kupigwa risasi wakati Jeshi la Polisi likiwatawanya waandamanaji wa CHADEMA, Kinondoni Jijini Dar

Mnamo February mwaka huu Jeshi la Polisi ililitoa taarifa ya kuwashikilia askari wake sita na silaha zao kwa ajili ya uchunguzi kuhusu tukio la kuuawa kwa risasi mwanafunzi Akwilina Akwilini

Aidha, tarehe 20 Aprili Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP), Biswalo Mganga alitangaza kulifunga jalada la uchunguzi wa kifo cha Mwanafunzi huyo Akwilina

Hata hivyo DPP alipoulizwa kuhusu Askari waliokamatwa baada ya kutokea kwa tukio la mauaji ya Akwilina alisema, “kama jalada nimelifunga, kwa hiyo askari wale nao wameachiwa huru hawana hatia.”

No comments:

Post a Comment