Almas Mzambele Afunguka na Kudai Babu Tale Ataiua WCB - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 27 July 2018

Almas Mzambele Afunguka na Kudai Babu Tale Ataiua WCB

Almas Mzambele ambaye alikuwa mfanyakazi wa WCB kwa miaka mingi kabla hajaonekana amefunguka na kudai mtu pekee ambaye ataiua WCB ni Meneja Babu Tale.

Almasi Mzambele alikuwa mtu ambaye alikuwa anashughulikia mambo ya mitandao ya kijamii WCB amefunguka kwa mara ya kwanza tangu ameondoka kwenye Label hiyo.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Almas amefunguka mazito juu ya uongozi wa kampuni hiyo ambao ndio amedai una matatizo zaidi na unaweza kuua Label hiyo.

Tatizo pale lipo  kwenye uongozi wa WCB ambapo mwenye matatizo zaidi ni Babu Tale anayejiita meneja namba moja yaani anavuruga watu mpaka wanaacha kazi sio mchezo.
Babu Tale ndio mtu anayepelekea kuiua WCB kuna vitu vingi anakuwa anavifanya nyuma ya pazia ambavyo kama watu wangevifahamu sidhani kama wangetamani kumuona yeye anaendelea kuwa na Diamond kwa sababu naamini huko mbeleni sidhani kama tutaendelea kumuona Diamond huyu tunayemuona sasahivi”.

Lakini pia Almas aliendelea kutaja maovu ya Babu Tale:

Yaani kifupi tu Babu Tale ni mbinafsi na ni mmwinyi anapenda yeye ndio aonekane msemaji wa mwisho k a sababu ndio ametangulia kufahamiana na Diamond kwaiyo mkitofautiana mtazamo tu basi yeye anaanza kuleta visa vyake”.

No comments:

Post a Comment