Zipo Kampuni Nimefanya Kazi, Mikataba Ninayo Wamekimbia na Hela Zangu- Mzee Majuto - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 27 June 2018

Zipo Kampuni Nimefanya Kazi, Mikataba Ninayo Wamekimbia na Hela Zangu- Mzee Majuto

 Staa mkongwe kwenye tasnia ya uigizaji nchini Mzee Majuto ambaye alikuwa nchini India kwaajili ya matibabu na amerejea nchini baada ya kumaliza matibabu.

Moja ya jambo ambalo ameliongelea King Majuto ni kuhusiana na kampuni ambazo aliwahi kufanya nazo kazi za matangazo na hawakumlipa anavyostahili au walivyokubaliana.

Mzee majuto amesema kuwa japo ana hela nyingi ambazo amezulumiwa kwa baadhi ya watu aliofanya nao kazi yeye ameawasamehe japo kuna hela nyingi zipo mikononi mwa watu na hawana mpango wa kulipa.

"Nimeletwa duniani kwaajili ya kuwachekesha watu na sio kuwapa laana watu kwahiyo nimewasamehe wote ambao wamenidhulumu pesa zangu mungu atawaonyesha hapa hapa duniani" Mzee Majuto.

No comments:

Post a Comment