YUSSUF AINYIMA UHONDO DENMARK KUCHUKUA ALAMA MBILI ZA ZIADA, YAENDA SARE NA AUSTRALIA KOMBE LA DUNIA - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 21 June 2018

YUSSUF AINYIMA UHONDO DENMARK KUCHUKUA ALAMA MBILI ZA ZIADA, YAENDA SARE NA AUSTRALIA KOMBE LA DUNIADakika 90 zimemalizika huko Urusi katika michuano ya Kombe la Dunia kwa Denmark kwenda sare ya bao 1-1 na Australia.


Mabao ya mchezo huo yamefungwa na Christian Eriksen mapema kabisa mnamo dakika ya 7 kipindi cha kwanza kwa upande wa Denmark. 

Bao la Australia limewekwa kimiani na Mile Jedinak kwenye dakika ya 38 kwa njia ya penati ikiwa ni baada ya Yussuf Poulsen kuunawa mpira katika eneo la hatari na kusababisha kupewa kadi ya njano.

Matokeo haya yanaifanya Denmark kuendelea kushika nafasi ya kwanza kwenye kundi C ikijikusanyia alama 4 huku Australia ikiwa na alama 1 katika nafasi ya 4.

No comments:

Post a Comment