YANGA KUANZA KAZI RASMI LEO KUWAWINDA GOR MAHIA - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 26 June 2018

YANGA KUANZA KAZI RASMI LEO KUWAWINDA GOR MAHIA


Na George Mganga

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuanza mazoezi leo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC kutoka Kenya.

Mazoezi hayo yanatarajiwa kuanza leo baada ya wachezaji wote wa Yanga kpewa mapumziko mapema baada ya kumalizika kwa mashindano ya SportPesa Super Cup yaliyokuwa yanafanyika nchini Kenya.

Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Mkongomani, Mwinyi Zahera, naye tayari amesharejea nchini tayari kuwaandaa Yanga kuelekea mechi hiyo ambayo Yanga inapaswa kupata matokeo ili kujiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele.

Ikumbukwe Yanga ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya MC Alger ya Algeria na kisha baadaye kwenda sare ya mabao 1-1 na Rayon Sports ya Rwanda hivyo kuzidi kujiwekea mazingira ya kuelekea hatua inayofuata.

Mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi hapa nchini itapigwa nchini Kenya Julai 18 2018 ukiwa ni mchezo wa mkondo wa kwanza.

No comments:

Post a Comment