Wimbo wa Iyena Umechangia Asilimia 98 Kumrudisha Zari Kwa Diamond....Soma Hapa - Karafuu24 Blog

Breaking

Sunday, 10 June 2018

Wimbo wa Iyena Umechangia Asilimia 98 Kumrudisha Zari Kwa Diamond....Soma Hapa

MWENYE nyumba kafufuka na nyumba ya mirathi haiuzwi tena, pole Hamisa Mobeto! Waswahili bhana, wao wape kichwa cha habari na habari yote watakuandikia…Ha! Ha! Haaa!

 Kama ninawaona vile wanavyocheka kwa ‘dharaaau’ pale mrembo Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ mzazi mwenza na mwanamuziki, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, atakapotua Madale, kwenye makazi ya mwanamuziki huyo.

 Halafu pia ninajiuliza mwanamitindo, Hamisa Mobeto, mzazi mwenza pia na Diamond, ambaye hivi karibuni alionekana kufurahia penzi la mwanamuziki huyo atazungumza nini juu ya suala hili.
Mengi ninajiuliza. Lakini nikuhakikishie mpenzi msomaji, maneno yale ya kwanza kabisa juu si yangu. Ni ya mashabiki wa Diamond ambao wanapenda kumuona akiwa kwenye uhusiano na Zari.

 Maneno hayo yameibuka baada ya kuonekana kuwa kuna kila dalili za wawili hao ambao walikuwa wamepigana chini kurudiana, baada ya meneja wa Diamond na familia ya mwanamuziki huyo kufanya jitihada za kumrudisha Zari kwenye familia hiyo.

Hata hivyo pamoja na yote yanayoendelea na hatua zinazochukuliwa kumrudisha Zari kwenye ‘White House’ ya Diamond huko Madale, niamini mimi Wimbo wa Iyena wa Diamond umechangia kwa asilimia 98 kumrudisha Zari kwa Diamond.

KIVIPI?
Hili ndilo swali la msingi unaloweza kujiuliza, si ndiyo? Sasa ipo hivi; Baada ya wimbo ambao Diamond kamshirikisha Rayvanny, kutoka na Zari kuonekana kashiriki kwa asilimia kubwa kwenye upande wa video, mashabiki wengi walianza kukomenti kwenye ukurasa wa Diamond, Instagram na meneja wake Babu Tale kwamba wanamtaka Zari, Madale.

BABU TALE ACHUKUA HATUA
Baada ya komenti kuwa nyingi Instagram, hiki ndicho Babu Tale aliandika; “Naona watu mnania-ndikia niwarudishe Mr and Mrs Dangote, hili kwangu ni kama kumsukuma mlevi yaani ni kazi ndogo sana.
“Ila Niliwaacha tu kwanza kila mtu sumu na hasira za mioyo yao ziwaishe ili wakirudiana akili iwakae sawa, sasa naona muda muafaka wa kulitumia jina langu ipasavyo, kama ambavyo mama Tee ananiita “Godfather”, siendi na magoti wala kutambaa nitapanda ndege kwenda hadi SA (Afrika Kusini) kuongea na mtu mzima mwenzangu na ninaamini yataisha kwa asilimia 100, wananzengo niende nisiende?”


Baada ya posti hiyo Instagram, Juni 2, Babu Tale aliposti picha akiwa uwanja wa ndege na kuweka wazi kwamba safari ya Sauz ilikuwa imewiva. Baadaye aliposti picha akiwa na Zari, Sauz. Nguvu ya Iyena inafanya kazi!

 MAMA DIAMOND NAYE HAYUPO NYUMA!
Mama wa mwanamziki huyo si habari ya kukushangaza kwamba anampenda Zari. Ni jambo ambalo linajulikana kwa wengi na hafichi mapenzi yake kwa mrembo huyo mwenye asili ya Uganda.

 Baada tu ya Wimbo wa Iyena kutoka, mama Diamond amekuwa akitupia picha mbalimbali kutoka kwenye video ya wimbo huo pamoja na vipande vya video huku akiandika maneno ya kumsifu Zari. Picha ya kwanza ya Zari aliyoposti baada ya Iyena kutoka aliambatanisha na maneno yaliyosomeka hivi; “#Mama Latiffa mwenye IYENA yake, mwanamke usafi gaga kulisugua mume akirudi sharti viatu kumvua.

 NDUGU WA DIAMOND WENGINE VIPI?
Kwa upande wa ndugu wengine wa Diamond, akiwemo dada yake Esma, Wimbo wa Iyena pamoja na komenti za mashabiki za kuwataka wawili hao kurudiana ni kama zimechochea nao wazidi kuonesha waziwazi mapenzi yao kwa Zari.

 Kwenye akaunti ya Instagram ya Esma, Zari hakauki, mara kwa mara anamposti huku akiambatanisha kepsheni fupifupi zinazoonesha mahaba yake kwa Zari. Ni nguvu ya Iyena inafanya kazi!

HITIMISHO
Baada ya nguvu kubwa ya Wimbo wa Iyena kuenezwa na familia ya Diamond, kwenye mitandao taarifa zimeshaanza kuzagaa kuwa, Zari ametia mguu ndani ya Dar huku nyingine (sio rasmi) zikiwaonesha Diamond na Zari wapo chumbani.

MAKALA NA BONIFACE NGUMIJE

No comments:

Post a Comment