WAZIRI RIZIKI PEMBE AONGOZA MAPOKEZI YA WANAMICHEZO 170 KUTOKA MWANZA - Karafuu24 Blog

Breaking

Monday, 18 June 2018

WAZIRI RIZIKI PEMBE AONGOZA MAPOKEZI YA WANAMICHEZO 170 KUTOKA MWANZA

MSAFARA wa wanamichezo 170 kutoka Unguja na Pemba umerejea nyumbani Zanzibar wakitokea Butimba Mkoani Mwanza kwenye Mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Skuli za Sekondari Tanzania maarufu UMISSETA.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma pamoja na viongozi mbali mbali wa Wizara hiyo akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Michezo na Utamaduni Hassan Khaillah Tawakal waliwapokea kwa shangwe wanamichezo hao ambao waliiwakilisha vyema Zanzibar baada ya kurejea na makombe makubwa matatu.
Akiwapongeza wana michezo hao Waziri Pembe amesema vijana hao wanastahiki pongezi kwani walikuwa na wakati mgumu ndani ya mashindano wakiwa na swaumu zao lakini wamepambana na kufanikiwa kushindaa kwa baadhi ya michezo.
NA ABUBAKAR KHATIB HAJI

No comments:

Post a Comment