WAZIRI HAJI OMAR KHEIR AWATAKA MANISPAA YA MKOA KUWEKA KIPAOMBELE MIRADI YA USAFI. - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 20 June 2018

WAZIRI HAJI OMAR KHEIR AWATAKA MANISPAA YA MKOA KUWEKA KIPAOMBELE MIRADI YA USAFI.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA, SERIKALI ZA MITAA NA IDARA MAALUM ZA SMZ HAJI OMAR KHEIR AMEWATAKA WATENDAJI KATIKA MANISPAA ZA MKOA WA MJINI MAGHARIBI KUWEKA KIPAUMBELE KATIKA MIRADI YA USAFI WA MJI NA UENDELEZAJI WA HUDUMA ZA JAMII KWENYE MIPANGO YAO.
AKIZUNGUMZA NA WATENDAJI WA MANISPAA HIZO WAKIWEMO WAKUU WA WILAYA, MAKATIBU TAWALA WA WILAYA NA MKOA WA MJINI MAGHARIBI KATIKA MAJUMUISHO YA ZIARA YAKE ALIYOIFANYA KATIKA MAENEO MBALI MBALI YA MKOA HUO WAZIRI KHEIR AMESEMA KUFANYA HIVYO KUTASAIDIA KUUWEKA MJI KATIKA HALI YA USAFI NA SALAMA KWA AFYA ZA WAKAAZI WAKE.

AMESEMA KATIKA ZIARA HIYO ILIYOANZIA KATIKA SOKO KUU LA DARAJANI NA KUPITIA KATIKA MASOKO YA MOMBASA, MWANAKWEREKWE NA KUMALIZIA KATIKA ENEO LA BUBUBU KWA NYANYA AMEWAAGIZA WATENDAJI HAO KUWEKA MIUNDOMBINU ITAKAYOLETA MASLAHI KWA WAFANYABIASHARA, WANANCHI NA SERIKALI KWA UJUMLA.
AMEWASISITIZA WAKURUGENZI WA MANISPAA HIZO KUFANYA UHAKIKI WA WAFANYABIASHARA WANAOTUMIA MASOKO HAYO NA KUWAPATIA VITAMBULISHO MAALUM VITAKAVYOWATAMBULISHA WAKATI WA UKAGUZI ILI KUWADHIBITI WATU WENGINE WASIOHUSIKA AU KUFANYA BISHARA ISIVYO HALALI.
KATIKA ZIARA HIYO PIA MHESHIMIWA KHEIR ALIWAAGIZA VIONGOZI ALIOAMBATANA NAO KUTUMIA SHERIA NA KANUNI ZA UTUMISHI WA UMMA, SERIKALI ZA MITAA NA TAWALA ZA MIKOA ILI KUWADHIBITI WATU WANAOWASIMAMIA NA WENYE TABIA ZA KUTOWAJIBIKA AU KUTOZINGATIA MASHARTI YA USAFI NDANI YA MANISPAA HIZO.
AIDHA WAZIR KHEIR ALIWATAKA WAFANYABIASHARA KATIKA MASOKO HAYO KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA MABARAZA YA MANISPAA KWA KULIPA USHURU NA ADA MBALI MBALI ZILIZOWEKWA ILI KUJENGA UWEZO WA MANISPAA HIZO KUTOA HUDUMA BORA NA KUYAENDELEZA MASOKO HAYO.

AKITOA MAELEZO KUHUSU AHADI YA KUWAHAMISHIA KATIKA ENEO LA KAMA WAFANYABIASHARA WA DAGAA WALIOPO KATIKA ENEO LA MARUHUBI, KATIBU TAWALA WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI HAMIDA MUSSA KHAMIS AMESEMA OFISI YAKE KWA KUSHIRIKIANA NA MANISPAA ZA MJINI NA MAGHARIBI ‘A’ ZINAENDELEA NA URATIBU WA SUALA HILO NA KWAMBA NDANI YA KIPINDI CHA MWEZI MMOJA UTEKELEZAJI WAKE UNATARAJIWA KUKAMILIKA
NA FATUMA MOHAMMED

No comments:

Post a Comment