WANAUME WATAKIWA KUWASAIDIA WANAWAKE KTATIKA KILIMO CHA MWANI - Karafuu24 Blog

Breaking

Thursday, 21 June 2018

WANAUME WATAKIWA KUWASAIDIA WANAWAKE KTATIKA KILIMO CHA MWANI

Wanaume wametakiwa kuwasaidia Wanawake Kilimo cha Mwani katika Maji ya kina kirefu ili kupata Mwani wenye bei nzuri na kuweza kujikwamua na Tatizo la Umasikini linalowakabili Wanawake hasa wa Vijijini.
    Amesema Mwani aina ya Kotonii umekuwa na bei nzuri lakini unahitaji kulimwa katika maji ya kina kirefu jambo ambalo linahitaji mashirikiano ya pamoja baina ya Wanawake na Wanaume  hasa kwa wanaume kuzamia katika maji ya kina kirefu kwa kuupanda mara akina mama wanapomaliza kuufunga.
     Akizungumza na Wakulima wa zao la Mwani katika Semina ya kuwajengea Uwezo wana vikundi wa zao la Mwani huko Mbweni Wilaya Magharib B Mwenyekiti wa Kongani Zanzibar Dr. Flora Ezekel Msuya amesema wanapoamua kutoa Mafunzo hayo na kuwashirikisha Wanaume ili kuwe na mashirikiano ya katika wa Wanawake na Wanaume na kuweza kufikia lengo lililokusudiwa.
     Amesema Wanawake wa Zanzibar wamekuwa wakilima Mwani katika Maji ya kina Kifupi kutokana na kutokuwa na nyenzo za kutosha hali ambayo inapelekea kutofikia lengo la Wajasiriamali hao kujikwamua na tatizo la umasikini.
     Amebainisha kuwa Wanaume wataweza kuzamia Maji ya kina kirefu  na kuupanda mara baada ya Wanawake wanapomalizi kuufunga na kuwarahishia kazi kwani sio wanawake wengi wanaoweza kuzamia Maji katika kina kirefu.
    Tunataka Wanaume washirikiane na Wanawake katika ukulima wa Mwani sio kuwapokonya alisema Dr. Flora
    Ametoa Wito kwa kwa Wanajamii na Wakulima wa zao la Mwani walime zao la Mwani wa kina kirefu kwani unaweza kupatia kipato katika familia zao na Taifa kwa ujumla ila kitu cha kuzingatia ni kufanya kazi kwa bidiii , kuzalisha bidhaa za Mwani zenye kiwango kinachokubalika.
   Ameeleza kuwa Wajitahiti kufuata masoko ya nje na ndani kwa ajili ya Wajasiriamali kupata kuuza bidhaa wanazozizalisha na kuepukana na kuzalisha biashara zisizokuwa na kiwango na kupelekea kupata hasara.
     Mweyekiti huyo ameema wameanza kuwafundisha Wajasiriamali kulima Kilimo cha Mwani tangu mwaka 2009 na kuwaletea wataalamu mbali mbali ili kutengeneza bidhaaa zinazokubalika.
       Ameendelea kusema kuwa Wamebaini wajasiriamali wengi wa Zanzibar wamekuwa wakitengeneza bidhaa lakini zimekuwa zikiharibika mapema na ndipo wakaaamua kutafuta fursa ya kuwa bidhaa wanazozizalisha zikae kwa muda mrefu na zisiharibike ambapo itawasaidia kupeleka bidhaa zao kwenye maonyesho na Masoko ya nje na ndani.
  Wamewaamua kufanya mawasiliano na na bodi ya chakula na vipodozi ili waje watowe mafunzo yatakayoziwezesha bidhaa kuwa na kiwango ili wazalishe bidhaa zenye viwango vya hali ya juu.
      Dkt. Msuya ambae ni mtafiti wa masuala ya Mwani Zanzibar amesema Mwani wa Zanzibar upo katika hali ya uzuri katika soko la dunia na wamemleta mtaalamu kutoka Indonesia kama vile Tambi,Makwaru,Visheti na Chauro.ukilinganisha na nchi nyengine ambazo zinalima mwani duniani.
   Amesma tatizo kubbwa linalojitokeza ni kubata matatiozo ya mabadiliko ya tabia ya nchi,na kuna mwani wa aina mbili kotonii ambao hauoti katika kina cha maji kidogo ambao ni wabei kubwa na na smosamu ni wa elfu moja kwa kilo ana gtz
     Amewataka wakulima wa mwani walime katika kina kirefu kwani wa kina cha chini maji amesema changamoto kubwa ambazo zinauthiri mwani wa zanzibar ni pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi na mabadiliko ya hali ya hewa yakitoko mwani unaunguwa naq kusinyaahasa wakati wa mvua nyingi.
Mapema wakitoa maelezo Safia Hashimu Makame na Hadia Ali Salim ambao ni Wanachama wa Kongano wamesema wanahitaji kushiriki kwa wingi kulima na kutengeneza Bidhaa zinazotokana na Mwani lakinui tatizo kubwa ni ukosefu wa Wafadhili, Masoko ya kudumu ya kuuzia Bidhaa wanazozizalisha na vitendea kazi.
     Aidha wameipongeza Taasisi hiyo kwa alimu walioitoa na kusema imeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa kuzalisha Bidhaa zenye kiwango ukilinganisha na walivyokuwa hapo awali.

No comments:

Post a Comment