Wakazi Akiri Hakuna Msanii Kama Davido - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 26 June 2018

Wakazi Akiri Hakuna Msanii Kama Davido

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Wakazi Music amefunguka na kumnyanyulia mikono msanii kutoka Nigeia David Adeleke maarufu kama Davido baadae ya ushindi wake wa tuzo ya BET.

Davido aliibuka mshindi wa tuzo ya BET 2018 katika kipengele cha ‘Best International Act’, tuzo zilizofanyika katika ukumbi wa Microsoft Theater huko mjini Los Angeles, jimboni California, Marekani.

Baada ya ushindi huo Davido alitoa hotuba ambayo ilikuwa imejikita katika kutangaza soko la Muziki wa Africa na kuwataka wasanii wa Marekani kufika Africa Kutembea:

Hotuba hiyo Ikiwa huwa watu wengi na mmoja wao ni Msanii Wakazi ambaye alishindwa kujizuia na kumwagia sifa lukuki Davido kwa hotuba hiyo ambapo kipitia ukurasa wake wa Instagram aliandika:

Hongera nyingi zimwendee Davido kwa ushindi wa “Best International Act” kwenye @betawards huko Marekani. Mwaka huu hakukuwa na mtanzania Ila pia Category ya International iliunganiswa Africa na Europe, so angechukua mwafrika yeyote tungehesabu Ushindi. Ila kikubwa ni kwamba mwaka huu ndio mara ya kwanza Tuzo za International kupokelewa on the Main Stage. Na niseme ukweli Davido hajatuangusha kwenye Speech yake. Ilikuwa Fupi and I understand maana sio mchezo (kutembea tu kwenda pale mbele unamuona kila Star, hatari) lazima utetemeke. Ila Davido alimshukuru D’banj kama Msanii aliyeanza kutufungulia milango african artists upande wa marekani (Collabo na Snoop Dogg, Signed by Kanye West) na pia alichukua Fursa kutoa salamu za rambirambi kwa familia ya D’Banj Maana amefiwa na mwanae (R.I.P Daniel III). Kisha akashukuru Fans, Familia yake, Management yake. Mwisho akawasihi wanyamwezi kuja africa wajionee hali, chakula na kufanya Collabo na Wasanii wetu, pia akasema Album yake inakuja soon. Kiukweli I don’t see any other artist kufanya a better job of representing zaidi ya alivyofanya OBO.
Ila sasa hii iwe changamoto na chachu ya sisi huku kupigania muziki wetu na sisi maybe tuje kushinda na kupata fursa ya kuinadi Tanzania kikamilifu. I know I’m inspired and I’m going to the studio leo. Ikiwezekana tuongeze support ya wenyewe kwa wenyewe kama itasaidia. Tuache UMBEA na kuongelea yasiyotuhusu, Tuache Uvivu… tupige Kazi, uwe underground uwe Legend!! Wote tuna nafasi… peace #AfricaPride

No comments:

Post a Comment