Waendelee Kushinikiza Wafanyakazi Wao Wasipige Nyimbo Zetu na Sisi Tunawakataa- Babu Tale - Karafuu24 Blog

Breaking

Wednesday, 20 June 2018

Waendelee Kushinikiza Wafanyakazi Wao Wasipige Nyimbo Zetu na Sisi Tunawakataa- Babu Tale

Wasanii wa  kundi la  WCB wamezungumza kuhusu baadhi ya vyombo vya habari kutopiga nyimbo za wasanii wao.

Miongoni mwa mameneja wa WCB, Babu Tale  katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam  jana alisema kwa vile vyombo hivyo viliwakataa mwanzo na sasa waendelee hivyo hivyo.

‘Tunaendelea kuwaomba waendelee kushinikiza wafanyakazi wao wasipige nyimbo zetu..

“Hatutaki kuona wanapiga nyimbo zetu wala kutoa habari zetu kwa sababu wao walitukataa mwanzo, tunawakataa kwa sababu wao walitukataa,” alisema Babu Tale kwa msisitizo.

Hapo awali Diamond Platnumz alisema siku zote katika tasnia mbalimbali michezo ya kubaniana ipo ila hawezi kulaumu.

Diamond  alisema kufuatia hatua hiyo iliyochukuliwa na vyombo hivyo  iliwapa nguvu timu nzima ya Wasafi kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuwasaidia wasanii wengine ambao wanakutana na changamoto hiyo.

No comments:

Post a Comment