VITA YA KOMBE LA DUNIA LEO NI HATARI TUPU, MISRI VS URUGUAY, URENO VS SPAIN - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 15 June 2018

VITA YA KOMBE LA DUNIA LEO NI HATARI TUPU, MISRI VS URUGUAY, URENO VS SPAIN


Baada ya wenyeji Urusi kufungua michuano ya Kombe la Dunia kwa kuwapa kipigo cha mabao 5-0 Saudi Arabia, leo inaendelea tena kwa viwanja vitatu kuwaka moto nchini humo.

Misiri watakuwa na kibarua chao cha kwanza dhidi ya Uruguay katika mchezo ambao utaanza majira ya saa 9:00 alasiri kwenye Uwanja wa Ekaterinburg.

Kuelekea mechi hiyo, nyota Mohamed Salah anapewa nafasi kubwa ya kukiongoza kikosi chake baada ya kupona majeraha yake ikiwa ni tangu aumie katika mchezo wa fainali ya UEFA Champions League wakati akikitumikia kikosi cha Liverpool dhidi ya Real Madrid.

Wakati huo Morocco ambao nao wanaiwakilisha Afrika watakuwa wanacheza na Iran, mechi itakayoanza saa 12 kamili jioni kwenye Uwanja wa St. Petersburg.

Mechi nyingine kubwa inayosubiriwa kwa hamu zaidi na wadau wengi wa soka duniani ni mabingwa wa taji hilo mwaka 2010, Spain watakuwa wanacheza dhidi ya Ureno kuanzia saa 3:00 usiku.

Mechi itakuwa inamkutanisha Ronaldo dhidi ya wachezaji wengi wengi ambao anacheza nao kwenye La Liga akiwemo Sergio Ramos ambaye ni nahodha wake ndani ya Real Madrid.

No comments:

Post a Comment