Vilio Vyatanda Mazishi ya Watu 6 wa Familia Moja Kati ya 14 Waliokufa kwa Ajali Mkuranga - Karafuu24 Blog

Breaking

Tuesday, 26 June 2018

Vilio Vyatanda Mazishi ya Watu 6 wa Familia Moja Kati ya 14 Waliokufa kwa Ajali Mkuranga

SIMANZI imetawala katika eneo la Ngunguti wilayani Mkuranga mkoani Pwani ambako watu 10 wa familia moja ni kati ya 14 waliofariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea jana eneo la Dundani.Ajali hiyo ilihusisha lori lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mkuranga kupoteza mwelekeo na kugongana uso kwa uso na Toyota Hiace iliyobeba abiria 18 waliokuwa wakielekea Msata kwenye mahafali.Wakizungumzia ajali hiyo ndugu wa marehemu wamesema kuwa wamepokea kwa majonzi taarifa za vifo vya ndugu zao huku wakisema tukio hilo si la kwanza kutokea katika eneo hilo hivyo kuwataka madereva kuwa makini.Mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo Mohammed Rashidi ameeleza kisa cha ajali hiyo Hata hivyo Mwenyekiti wa Kitongoji cha kiloweko Omary Hamza ametoa ushauri kwa madereva wa magari makubwa kuzingatia sheria za usalama wa barabarani kutokana na wengi wao kuwa wabishi.

No comments:

Post a Comment