Utata Mzito Waibuka Msiba wa Sam wa Ukweli Ndugu zake na Meneja Wake Hapatoshi - Karafuu24 Blog

Breaking

Friday, 8 June 2018

Utata Mzito Waibuka Msiba wa Sam wa Ukweli Ndugu zake na Meneja Wake Hapatoshi

KUFUATIA kifo cha msanii wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli kilichotokea usiku wa kuamkia jana Alhamisi, utata mzito umeibuka katika Hospitali ya Mwananyamala ambapo mwili wa marehemu uliifadhiwa kwa kusubiri ratiba za maziko.Ndugu wa marehemu waliamua kuingilia kati baada ya kutoona ushirikiano wa watu ambao walikuwa wamepata ahadi ya kufanikisha baadhi ya gharama za maziko hayo wakiwemo Mameneja wake wa zamani ambapo ni Papaa Misifa, Meneja Maneno, Meneja Kisaka na wasanii wenzake.Hata hivyo ndugu hao walichukua uamuzi huo baada yakukata tamaa tena kwa kutoona ushirikiano wa asilimia hata 75 kwa wasanii wa muziki na kama ilivyokuwa kwenye misiba ya wasanii wengine.Utata huo uliisha baada ya wahusika hao kufika eneo la tukio na kufanikisha kwa haraka malalamiko hayo.

No comments:

Post a Comment